Monday, May 7, 2012

.........VICTORIA BECKHAM AMSAHAU MWANAYE......


FASHENISTA Victoria Beckham ametoa kali ya mwaka baada ya kumsahau nyumbani kijana wake mmoja ambaye alipaswa kumpeleka shuleni.

Victoria anasema aliamka asubuhi kwa lengo la kumpeleka shule mtoto wake Brooklyn mwenye umri wa miaka 13, lakini alijikuta ndani ya gari yupo yeye na binti yake mdogo, Harper mwenye umri wa miezi kadhaa.

"Niliangalia kwenye siti za gari na kuona kuna kitu kimekosekana, nikiwa naendesha huku nafikiria nimesahau nini, nikakumbuka Brooklyn hayupo ndani ya gari, kumbe nilimuacha jikoni akinywa chai," anasema Victoria.

Mwanamke huyo mwenye watoto wanne anakiri kuwa ni msahaulifu sana na hii imetokana na kuwa na kazi nyingi, kwani ni mama, mfanyabiashara, mwimbaji na mbunifu wa mavazi. Anasema kazi hizi humfanya awe bize wakati wote.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms