Wednesday, May 23, 2012

........UCHEKESHAJI HAUNILIPI SANA - SHARO MILIONEA.......


MCHEKESHAJI mahiri katika tasnia ya uchekeshaji ya Swahiliwood, Hussein Mkiety Sharo Milionea, amesema kuwa sanaa ya uchekeshaji kwake hailipi kama inavyolipa kwa wengine.

Anasema hadi leo bado hajaona fedha yake tofauti na muziki anaofanya ambao ndiyo anakiri unamwingizia kipato.

Kwangu mimi sanaa ya uchekeshaji hailipi tofauti na muziki, kwa sasa nina vibao vitatu tu lakini mafanikio yake nayaona," alisema
.
"Kweli uchekeshaji umenipa umaarufu, lakini fesdha yake ni ya muda tu kwa sababu uigizaji kazi inakuwa siyo yako ni mali ya mtayarishaji kwa hiyo wewe unakuwa hauna chako tena, anasema.

Sharo Milionea ambaye amekuwa maarufu kutokana na staili yake anayotumia katika kuigiza, amesema kupitia muziki kuwa amefanikiwa kusafiri nje ya nchi na kufanya maonyesho na kulipwa vizuri na bado anaendelea kupata mialiko zaidi.

Hata hivyo anakiri kuwa kuna baadhi ya wasanii wa kuchekesha ambao wamefaidika na uchekeshaji na kuweza kupata fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms