Wednesday, May 9, 2012

....UCHE JOMBO NA MASTAA WENZAKE WAJIKUTA NDANI YA KITUO CHA POLISI JIJINI LAGOS.....


HAKUNA cha staa wala nini lazima mlale selo mkivunja sheria za nchi. Ndiyo mambo yaliyowakuta mastaa wa Nollywood, Uche Jombo, Van Vicker, Uduak Isong na wengine wakajikuta ndani ya kituo cha Polisi jijini Lagos Alhamisi iliyopita.

Habari zinasema wasanii hao walinaswa wakipiga picha za filamu kwenye eneo la Surulere, Lagos na watu wengine. Walishikiliwa kwenye kituo cha polisi cha Bode Thomas, Surulere, Lagos.

Habari zinasema kuwa wasanii hao walikamatwa kwa kosa la kupiga picha za filamu kwenye maeneo ya kituo hicho cha polisi bila idhini ya jeshi hilo na walikuwa wakitengeneza filamu ambayo inaelezea makosa na ukatili wa askari kwa raia.

Chanzo kinasema kuwa wasanii hao walioshikiliwa kwa muda wa saa 12 na kutoa maelezo ya kujitosheleza, walipewa kibali na askari mmoja ambaye hakuwa na mamlaka na hata walipokamatwa alikuwa akiwaangalia tu.

Hata hivyo, madai mengine yanasema kuwa Polisi wamekuwa na bifu na wasanii hao kwa vile wamekuwa wakifanya mambo ya kufichua siri na mambo mabaya ya kila siku ya polisi kwenye filamu zao.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms