Thursday, May 24, 2012

.....UCHE AMNASA MZUNGU.....


KARIBU wiki kadhaa baada ya ndoa ya waigizaji mastaa wa Nollywood, Stephanie Okereke na Linus Idahosa, iliyofuatiwa na ile ya Chidi Mokeme, kengele zinagonga tena.
Safari hii mwigizaji mwingine, Uche Jombo, kwa siri amefunga ndoa na mpenzi wake Mmarekani, Rodriguez mjini New York.
Habari za ndoa hiyo iliyowashangaza wengi zimekuja wiki kadhaa baada ya tetesi kuenea kuwa mzaliwa huyo wa Abiriba, Jimbo la Abia, anajiandaa kuolewa na Mfanyabiashara wa Marekani aitwaye Chidi.
Kwa hali yake ya kindoa ya sasa, watu wa karibu na mwigizaji huyo wamesema staa huyo aliyeshinda tuzo nyingi atahamia Marekani moja kwa moja.
Uche aliyeibukia katika tasnia ya filamu za Nigeria mwaka 1999 alipoigiza kwenye 'Visa To Hell', tangu hapo amekuwa na mafanikio makubwa akishiriki katika filamu 100.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms