Wednesday, May 23, 2012

.......SIKUCHUKIZWA NA UTARATIBU WA UTOAJI TUZO......


MWIGIZAJI wa muda mrefu, Justus Esiri, amekanusha taarifa kuwa alikasirishwa kwa kukosa kutunukiwa tuzo ya taifa.

Mwezi mmoja uliopita, iliandikwa katika mtandao kuwa msanii huyo hajafurahishwa na kukosa tuzo wakati wenzake kama Stephanie Okereke na Genevieve Nnaji wamekuwa wakituzwa mara nyingi.

Taarifa hiyo ilimkariri akisema: "Nimehuzunishwa sana kwani katika kazi zote nilizofanya, sijawahi kupewa tuzo, wakati walioshiriki kwenye vipande tu vya filamu za Samanja, New Masquerade na Yoruba wamepewa tuzo.

Esiri, aliyeonekana kushitushwa na taarifa hizo, anasema hizo ni habari za uongo.
Nilishawahi kutuzwa, sijawahi kulalamikia tuzo hizi, watu wanajiandikia tu mambo, wanazusha lolote," alisema.

Staa huyo aliibukia kuwa maarufu baada ya kuigiza katika mchezo wa televisheni wa 'Village Head Master' na alishawahi kupata tuzo.
Amecheza filamu nyingi za Nollywood zikiwamo Corridors Of Power, Last Knight, The Tyrant na The Investigation.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms