Monday, May 28, 2012

......SHARONI STONE NI MBAGUZI.....


MWIGIZAJI, Sharon Stone, amefikishwa mahakamani na aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani, akimtuhumu kumfanyia vitendo vya kibaguzi wakati akifanya kazi nyumbani kwake.

Mfanyakazi huyo, Erlinda Elemen, ambaye ni Mfilipino, amemshtaki mwigizai huyo mwenye umri wa miaka 51 aliyewahi kuigiza katika filamu maarufu ya Basic Instinct.

Elemen anadai awali aliajiriwa na mwigizaji huyo kuwa Yaya wa mtoto wake mmoja kati ya watatu alionao, baadaye alipandishwa cheo na kuwa Yaya Mkuu mwaka 2008.

Alikuwa akisafiri na mwigizaji huyo kila alipokwenda na watoto wake mpaka alipofukuzwa kazi mwaka 2011.

Miongoni mwa mambo ya anayolalamikia mfanyakazi huyo ni kutakiwa kuzungumza Kiingereza cha Marekani kwasababu hakupenda alivyokuwa akizungumza.

Aidha anadai alimwambia kuwa Wafilipino ni wajinga na pia alimkataza kuingiza Biblia katika nyumba yake.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms