Thursday, May 3, 2012

SASA NIMERUDI KWA NGUVU NA KASI MPYA.....


MWIGIZAJI nyota wa filamu Swahiliwood, Alice Bagenzi Rayuu, alikuwa kimya katika tasnia ya filamu kwa sababu alikuwa bize na masuala yake binafsi, lakini sasa yupo anaendelea kama kawaida na lengo lake ni kujenga uwezo na kuwa na nguvu kama walivyo waigizaji wa kiume.

Kuna wakati unakaa pembeni ukisoma mchezo unakwendaje, ukirudi unakuja kwa nguvu zote, kwa sasa nafikiria kumiliki kampuni yangu mwenyewe ya utengenezaji wa filamu kama vile walivyo wasanii wakubwa wa kiume kama Ray na wengine, anasema.
Rayuu amesema katika tasni ya filamu hadi sasa hakuna mtayarishaji wa kike mwenye nguvu kama wanaume, hivyo yeye anataka achukue nafasi hiyo.
Anasema katika muziki hali hiyo imewezekana, na kwamba anafurahia mafanikio ya msanii kama Judith Wambura, Lady Jay D, hivyo anataka katika filamu awepo mtu kama huyo ambaye atatoa ajira kwa wasanii wa kike bila masharti magumu
.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms