Monday, May 14, 2012

.......RUSSELL AANAZA KUJUTIA MAAMUZI YAKE...


MCHEKESHAJI, Russell Brand, amemwandikia barua pepe mkewe wa zamani, Katy Perry, akijutia uamuzi wake wa kukubali kuachana naye miezi 14 tu tangu wafunge ndoa.

Brand amejilaumu kwa uamuzi wake wa kukubali kuachana na mwanamke huyo mapema mno bila kufanya juhudi zozote za kuiokoa ndoa yao.

Barua hiyo imekuja baada ya Perry kupigwa picha akiwa na mpenzi wake mpya, Robert Ackroyd, ambaye ni shabiki wa bendi ya muziki, The Machine.

Brand alifungua madai ya talaka mwishoni mwa mwaka jana kwa madai kuwa wamekuwa na tofauti ambazo haziwezi kurekebishika kwa namna yoyote ile.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms