Monday, May 14, 2012

......POMBE NA BANGI ZAMTESA RIHANNA....


ULEVI uliopindukia, umemfanya mwanamuziki Rihanna, alazwe katika hospitali moja huko New York mara tu baada ya kumaliza shoo ya Met Gala.

Rihanna ambaye sasa ndugu na marafiki wameanza kumshauri atafute matibabu kwa ajili ya kudhibiti ulevi huo, inaelezwa alizidiwa baada ya kunywa pombe kali na kuvuta bangi.

Lakini madaktari wanasema Rihanna alizidiwa kutokana na uchovu na kutumia ulevi ambao hawakuuainisha.

Marafiki wanasema wamemshauri mwenzao apunguze ulevi kwa kuwa unaweza kumfanya ashindwe kufanya kazi yake kwa ufasaha siku za usoni.

Lakini Rihanna amekataa akisema kuwa hawezi kuachwa kunywa na kuvuta kwani ndivyo vitu vinavyomfanya atafute pesa.

"Natafuta pesa ili nijinunulie kila ninachokihitaji, siwezi kuacha kuvuta wala kunywa," anasema Rihanna.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms