Monday, May 21, 2012

......NIKO TAYARI KURUDISHA HESHIMA YANGU.....


BAADA ya kupotea katika muziki kutokana na ulevi na kashfa mbalimbali, mwanamuziki Britney Spear, ameibuka na kusema yuko tayari kurudisha heshima yake, lakini mwonekano wake unazungumza tofauti.

Hivi majuzi alitambulishwa kuwa Jaji wa shindano kubwa la uimbaji, X Factor, ambapo alionekana mwenye wasiwasi.

Britney aliyekuwa mlevi wa kupindukia, alionekana akitafuna kucha mbele ya waandishi wa habari mpaka zikaanza kutoa damu hali iliyoashiria uoga.

Aidha alikuwa akikunja vidole muda wote wakati akiongea hali iliyoashiria kuwa alikuwa akiogopa kupita kiasi na kuwaacha watu wakihoji kama yuko tayari kurudi jukwaani kuimba.

Mwanamuziki huyo aliingia na Demi Lovato kuchukua nafasi za Paula Abdul na Nicole Scherzinger ambao wameondolewa katika safu ya majaji.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms