Wednesday, May 9, 2012

.....NIKO KWA OBAMA NAPIGWA MSASA.....


MWIGIZAJI mrembo, Nadia Buari yupo Marekani akipigwa msasa kwenye masuala ya uigizaji, marafiki zake wa karibu wamethibitisha.

Habari zinasema msanii huyo pia atatumia nafasi hiyo kukutana na mastaa mbalimbali wa Hollywood ambako ndiko alipokuwa akitaka kufanya kazi tangu siku nyingi.

Ingawa haijajulikana atamaliza lini mafunzo hayo, lakini imeelezwa kuwa msanii huyo amepania kufanya mambo makubwa na kujiweka kwenye levo ya tofauti na wasanii wengine wa kike wa Nollywood.

Nadia ambaye ni raia wa Ghana, amekuwa akifanya vizuri katika filamu za nchi zote mbili yaani Ghana na Nigeria. Maskani yake kubwa yamekuwa jijini Lagos ambako ana kazi nyingi.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms