Wednesday, May 23, 2012

....MKWARA WA AKI, ANUNUA MAGARI MAWILI KWA MPIGO KWA AJILI YA MKEWE....


NI ndani ya mwezi mmoja tu, mwigizaji maarufu wa Nollywood, Chinedu Ikedieze Aki, amemnunulia mkewe, Nneoma, magari mawili ya kifahari, moja ni Infiniti Jeep FX na jingine ni Honda Accord.

Kuongezea habari nzuri kuhusu yeye, msanii huyo mzaliwa wa Umuahia, Abia anayejishughulisha pia na ujasiriamali, amewaambia wanaomsema kwa kuishi nyumba ya kupanga kuwa si muda mrefu atahamia katika nyumba yake.

Habari zimethibitisha kuwa ujenzi wa nyumba yake ulioanza miezi michache iliyopita, tayari umeshafika asilimia 75.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kama mambo yataendelea kama yalivyo sasa, staa huyo atahamia katika nyumba yake kabla ya mwisho wa mwaka huu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms