Friday, May 18, 2012

........MISS EAST AFRICA ETHIOPIA HUYU HAPA......

Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wanaendelea kupatikana kutoka katika Nchi mbalimbali zinazoshiriki mashindano hayo.

Mrembo mwingine aliyeingia fainali ni Miss Lula Teklehaimanot (19) kutoka Nchini Ethiopia ambae alipatikana mwishoni mwa wiki baada ya kuwashinda warembo wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Ethiopia katika fainali hizo.

Miss Lula Teklehaimanot ana urefu wa 1.79m na uzito wa 52kg ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha St. Merry University cha jijini Addis Ababa, Ethiopia ampapo anasomea degree ya Marketing

Pia Mrembo huyo ni miongoni mwa wanamitindo maarufu wanaochipukia kwa kasi Nchini Ethiopia.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms