Saturday, May 5, 2012

.........MARIA CAREY NA KIVAZI CHA UTATA.....

KIVAZI cha supastaa, Mariah Carey kiliwafanya mashabiki waache kufuatilia anachoimba na macho yao wakayakodoa kwenye kivazi alichotilia siku hiyo ambacho kilimbana haswa.

Ingawa kivazi hicho kilivuta macho ya mashabiki lakini hakikumpa uhuru Carey pia kwani alionekana kuwa na wasiwasi na kukivuta vuta kila wakati.

Ilikuwa ni Mei Mosi na Carey alikuwa akiimba maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya watoto wake mapacha kutimiza umri wa mwaka mmoja, lakini 'skin tight' aliyovaa ilimfanya aonekane kama analia badala ya kutabasamu.

Hata hivyo ni kama alijua kivazi chake siku hiyo kilimpa tabu, alikiri kutojiandaa kwa kuwa na furaha kubwa ya watoto wake, Morocan na Monroe kutimiza umri wa mwaka mmoja.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms