Wednesday, May 23, 2012

..........LOLA AFUNGUKA.....


KUNA vitu vingi vya kujifunza na vinavyovutia kwa mwigizaji mahiri wa Nollywood, Lola Alao.

Si tu kwamba mwanadada huyo ana mafanikio, lakini pia hutoa kauli za maana katika tasnia hiyo.

Katika mahojiano ya hivi karibuni, mwigizaji huyo aliweka wazi changamoto alizokabiliana nazo siku za nyuma, namna alivyozishinda pamoja na mambo mengine.

"Kuna nyakati nilikuwa matatizoni, nilikabiliwa na changamoto nyingi...niliwahi pia kuvamiwa uwanja a ndege," alisema.
"Hakuna aliyesimama upande wangu. Kuna watu pia walikuwa wakinidai mno hadi nikalazimika kuuza gari langu ili kulipa madeni.

"Hata wale waliokuwa wakinifahamu, waliopaswa kuwa msaada kwangu, walinizunguka. Lakini yote nilimwachia Mungu.
"Ndiyo maana ninaamini kuwa kama kuna kitu cha kudumu duniani, ni mabadiliko.

"Ninamtukuza Mungu kwa mafanikio yangu, pia namshukuru na baba yangu, Kalejaiye, amekuwa upande wangu siku zote.
"Ndiye mtu pekee niliyemwona katika shida zangu, aliniambia nisihesabu nimeanguka mara ngapi, bali nihesabu nimesimama mara ngapi.

"Mungu alimtumia baba Kalejaiye kwa ajili yangu. Kila mara aliniambia, 'Lola, Mungu ameruhusu jambo hilo kukutokea ili umtukuze na utambue thamani yake.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms