MCHEZA filamu anayetamba kwenye ‘game,’ Jacob
Steven ‘JB’ (pichani) hivi karibuni alinusurika kuuawa na majambazi waliovamia
Pub ya msanii mwenzake, Aunt Ezekiel iliyopo eneo liitwalo Gereji Mwananyamala
jijini Dar.
Akizungumza na Ijumaa, JB alisema kuwa baada
ya majambazi hao kuvamia katika pub hiyo saa 5.30 usiku, hakuwastukia kama
walikuwa wahalifu bali alidhani ni wateja wa kawaida.
“Mimi sikuwashitukia kama wale watu walikuwa
majambazi, ila baada ya kutoa bastola na kutuamuru tulale chini na tutoe kila
kitu nikajua kimenuka, nikatimua mbio ambazo sijawahi kukimbia licha ya mwili
wangu huu,” alisema JB.
Aliongeza kuwa, wakati akitimua mbio
aliwasikia watu wakimuaru asimame lakini hakutii hadi alipofika Kituo cha
daladala cha Komakoma ndipo alisimama na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru na
kifo.
0 comments:
Post a Comment