Monday, May 14, 2012

......HATIMAYE BIEBER AMALIZA SHULE.....

MSANII kinda, Justin Bieber, hii imekuwa ni wiki nzuri kwake kwani ndiyo amemaliza elimu ya sekondari baada ya kuisotea kwa muda mrefu kutokana na kutingwa na muziki.

Bieber ameonyesha furaha yake ya kutua mzigo huo kwa kuandika kila mara katika mtandao kuwa anashukuru amefanikisha jambo hilo ambalo mama yake alikuwa akiling'ang'ania.

"Nimemaliza shule na kufaulu mitihani yangu vizuri, sasa niko huru kwani ilikuwa ngumu kwangu kufuata masomo na muziki kwa wakati mmoja," ameandika katika mtandao huo.

"Ninafuraha kwa kuwa nimefanikisha kile ambacho mama yangu alikuwa akiking'ang'ania sana, nilifanya hivi kwa ajili yake. Kiukweli nilikuwa siipendi kabisa shule."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms