Saturday, May 19, 2012

......BOB MARLEY KUENZIWA KESHO......

TAMASHA la kumuenzi hayati Bob Marley lijulikanalo kama (Carribean beat) linatarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Kijitonyama Posta kwa kuwashirikisha wanamuziki 55 wa muziki wa Reggae kutoka ndani na nje ya jiji la Dar es salaam.

Mkurugenzi na mwandaaji wa tamasha hilo, Benji Cosmo alisema tamasha hilo litaanza saa mbili usiku mpaka saa kumi na moja asubuhi lengo likiwa ni kuinua vipaji katika muziki wa reggae hapa nchini na kumuenzi hayati Bob Marley.

Alisema ni mara chache watu kuukubali muziki huo, lakini ukweli halisi wa muziki wa Regga ni barani Afrika hivyo sasa ni wakati wa Waafrika kukubali muziki wa asili yao.

"Wanamuziki 55 wanatarajiwa kupanda jukwaani na kutumbuiza miondoko mbalimbali ya muziki wa reggae, huku televisheni 'screen' kubwa zitakazokuwa zimefungwa uwanjani hapo zitawapa mashabiki nafasi ya kushudia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Bayern Munich na Chelsea."

Cosmo alisema katika kuboresha tamasha hilo wameamua kuweka kiingilio kidogo cha sh 5000/= na eneo la maegesho ya magari 100, pamoja na ulinzi wa kutosha kutoka kwa walinzi 40 watakaozunguka muda wote kuzuia uhalifu mahali hapo.

Aliwataja baadhi ya wanamuziki wakali watakaotoa burudani usiku huo kuwa ni washindi wa muziki wa katika tuzo za Kili award, Warriors Band kutoka jijini Arusha, Jhikoman, Ras Inno akiwa na Innocent people band, Ras Six The East Yellowman na Jahson Matungwa.

Naye Innocent N aliongea kwa niaba ya wanamuziki wenzake amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms