Monday, May 21, 2012

...TRAVOLTA .NDANI YA KASHFA NZITO......


STAA John Travolta ameingia kwenye kashfa nzito baada ya wanaume watatu kujitokeza wakidai kuwa mwigizai huyo aliwahi kuwaomba wafanye mapenzi.

Wanaume hao ambao wawili ni wafanyakazi wa saluni na mmoja wa meli, wamesema mwigizai huyo ni shoga kwa kuwa aliwahi kuwatamkia na kuahidi kuwapa pesa nyingi iwapo watamkubalia.

Hivi karibuni wafanyakazi wawili wa kiume katika saluni ya masaji, walisema mwanaume huyo aliwahi kuwafanyia vitendo ambavyo viliashiria kuwa ni shoga.

Mfanyakazi mwingine wa meli naye aliibuka na kudai kuwa Travolta aliwahi kumtamkia maneno ambayo yanaashiria kuwa ni shoga, huku akiahidi kumpa Dola 12,000 kama atakubali kufanya naye mapenzi.

Hata hivyo Travolta ambaye ni baba wa watoto wawili, hajajitokeza kuzizungumzia tuhuma hizo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms