Thursday, May 3, 2012

......BADO NIPO NIPO KWANZA.......BADO NIPO NIPO SANA.....

LIZZY haolewi ng'o, mtabaki kusubiri tu. Lizzy Anjorin amesema kuwa hataki kukurupuka kwa vile hataki mwanamume tegemezi na mtu asiye na malengo.

"Nataka mwanamume ambaye atakuwa bize na kazi, sitaki mtu wa kuzubaa zubaa na kuanza kusikiliza majungu ambayo marafiki zangu huwa wanaamua kunitungia tu kunichafua," alisema.

"Nikiingia kwenye ndoa itanibana nitashindwa kufanya mambo mengine, kwa hiyo lazima nichukue muda, siyo leo wala kesho."

Msanii huyo anasema kuwa watu wengi hushindwa kumuelewa kwa vile yeye ni mtu wa kupuuza mambo na kuendelea na maisha yake ingawa mara chache uzalendo humshinda.

Msanii huyo alikuwa akidai hivi karibuni kwamba kuna staa mwenziwe wa kike anamloga, ingawa washindani wake walidai kwamba hakukuwa na lolote bali alitaka tu kuandikwa magazetini.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms