Wednesday, May 16, 2012

......ANTI FIFI AIBUKA TENA......


MTUNZI wa filamu ya Senior Bachelor ambaye pia ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu za Swahiliwood, Tumaini Bigirimana Anti Fifi, ameamua kuiendeleza sehemu ya tatu ya filamu hiyo.

Senior Bachelor ndiyo filamu iliyomtangaza JB hadi kuibuka mshindi wa tuzo ya Mwigizaji Bora na pia filamu yenyewe kutwaa tuzo ya Filamu Bora.

Nimeamua kuiendeleza filamu hii kutokana na maombi ya watu, sasa sehemu ya tatu inakuja," alisema Aunt Fifi.

"Senior Bachelor ni filamu iliyotungwa vizuri sana na kukubalika, kuna wakati watu wanaamini kuwa uzuri wa filamu ni uigizaji wa mtu, kumbe si kwel.

"Hadithi nzuri ndiyo inamfanya msanii angare, kwa kuonyesha hilo Senior Bachelor inachezwa bila ya kuwepo JB na itafanya vizuri."

Awali filamu hiyo ilizua utata kuhusu nani aliyestahili kupata tuzo zilizotokana na filamu hiyo, huku JB akisema tuzo zilizopatikana zilikuwa ni zake wakati Anti Fifi aliwauliza watoaji wa tuzo hizo walitumia vigezo gani.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms