Monday, April 30, 2012

........WIMBO WANGU WA MAGUBEGUBE UNA UJUMBE MZITO.....


MSANII aliyesheheni vipaji lukuki kutoka Tanzania, Barnaba Elias Barnabas, amesema kuwa ujumbe uliomo katika wimbo wake wa Magubegube, ni mzito zaidi ya jina la wimbo wenyewe.

"Magubegube ni wimbo ambao nilipanga kuwapa ujumbe wanafunzi wa shule hasa wa kike," anasema Barnabas.
"Kuna wanafunzi ambao wanakwezwa na walimu wao baada ya kuwaridhisha kimapenzi, pia wapo ambao wanafelishwa makusudi hasa wanapokataa kuwaridhisha kimapenzi baadhi ya walimu wenye tabia mbovu.

"Lakini pia ujumbe huo unawaendea na wale wanaopenda ovyo na wenye tabia chafu za kutembea na wake za watu.

"Nilikuwa na mengi na mengine nilishindwa kueleza ndani ya wimbo huo, lakini nina imani umeelimisha vile ipasavyo."

Mwaka huu mwanamuziki huyo alibahatika kupata tuzo ya KTMA baada ya kushirikishwa katika tuzo hizo kwa miaka mitatu mfululizo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms