Thursday, April 5, 2012

....WASANII WAKUBWA NI WABINAFSI......

MWIGIZAJI na mtayarishaji katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, Simon Mwakipagata Kapturado, anasema katika tasnia ya filamu, wasanii wakongwe wamekuwa wazito kuwasaidia wanaoinukia.

Anasema alipata kufahamu hilo wakati akiandaa filamu yake ya I Think I Hate My Wife ambayo anasema imemtesa mno hadi kuingiza sokoni.

Umasikini umetufanya wasanii kuchukiana na hata kudharauliana, msanii akishajiona ana jina kubwa basi atakusumbua sana unapotaka kumtumia kwenye filamu yako," alisema.

"Katika maisha yangu ya utengenezaji filamu hakuna filamu iliyonitesa kama hii, nilizimia zaidi ya mara tatu kwa ajili ya msanii mmoja mkubwa, kila siku za kurekodi zilipofika hakuwa akitokea.

"Siku aliyokuja akanibadilikia kuhusu malipo na kudai fedha nyingi zaidi ya milioni moja kutoka makubaliano yetu ya awali.
"Nikazitafuta na kumpatia, aliondoka na hakurudi kwa siku mbili tukashindwa kurekodi, hata simu yake ikawa haipatikani."

Kapturado alisema siku ambayo msanii huyo alitokea hakuwa amekwenda na nguo alizotakiwa kuvaa kwa ajili ya kurekodi.
"Yaani jamaa alinivuruga kabisa katika bajeti, lakini nimejifunza."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms