Thursday, April 12, 2012

....TONTO DIKEH KWA KUBWATUKA HAJAMBO, ABWATUKA TENA......

NI takribani wiki mbili tu zimepita tangu mwigizaji Tonto Dike awape zawadi mashabiki wake baada ya kuwauliza maswali kupitia mtandao.

Dikeh alikuwa anawauliza maswali mashabiki wake katika mtandao wa twitter yanayomhusu yeye na kazi yake ya uigizaji na waliofanikiwa kujibu aliwapeleka katika hoteli moja ya nyota tano ambako walikula na kulala.

Wiki iliyopita, Dikeh alihojiwa na kituo cha televisheni na kuulizwa iwapo anaweza kuolewa na wanaume wa kabila lake la Igbo ambapo alisema haiwezekani kwa kuwa ni wambea.

Maneno hayo yalimkera shabiki wake mmoja aliamua kumjibu akimwambia ni mpumbavu, kwa kuwa hawezi kuwasema wanaume ambao ni kabila moja na la baba yake.

Haikuchukua dakika mbili kabla Dikeh hajaanza kumjibu na kumporomoshea matusi makubwa shabiki huyo, huku akisisitiza kuwa hiyo ni sababu nyingine inayomfanya asiwapende wanaume wa kabila hilo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms