Wednesday, April 25, 2012

.......TONTO DIKE AMELIKOROGA TENA......

PRODYUZA mmoja wa maeneo ya Asaba jijini Lagos, Nigeria, huenda akamshtaki msanii wa kike ambaye ni mtata, Tonto Dikeh baada ya kutotokea kwenye sehemu ya kupiga picha za filamu yao mpya.

Habari zinasema prodyuza huyo haelewi alipo msanii huyo ambaye kila akipigiwa simu haipokelewi. Lakini kuna maelezo kwamba alituma meseji kwamba anaondoka kwenda mjini kufanya mambo yake na sehemu yake ataifanya siku nyingine.

Prodyuza huyo ameshatoa taarifa kwa umoja wa wasanii wa filamu Nigeria na asiporejea eneo la kazi haraka iwezekanavyo atachukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kumkamata kwa Polisi.

"Huu ni utovu wa nidhamu Nollywood, alidai kwamba anaenda Lagos angerudi Jumanne lakini kimya. Kutokuwepo kwake kumetukwamisha sana," alinukuliwa prodyuza huyo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms