Friday, April 13, 2012

........RUKKY SANDA AKANA KUFANYA UPASUAJI.......

MWIGIZAJI wa Nollywood, Rukky Sanda amekanusha tuhuma za kuufanyia upasuaji uso wake lakini amesema hata kama angefanya hivyo ni kwa sababu ana pesa.

Tuhuma hizo zimekuja baada ya mwanamke huyo kurejea Nigeria akitokea Marekani ambako alikaa kwa muda wa takribani miezi miwili.

Sanda amesema labda anaonekana mzuri hivi sasa kwa sababu ana pesa na maisha mazuri huku akikanusha kufanya upasuaji.

Sijarekebisha chochote katika mwili wangu, labda nyie mnaona nimekuwa mzuri zaidi kwa sababu nimetoka kula raha, na hata kama nimefanya inabidi mnipongeze kwa kuwa siyo kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya, inahitaji pesa nyingi sana, anasema Sanda.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms