Monday, April 23, 2012

.......PETER MSECHU ANG'ATA, ASEMA MTOTO WAKE ASIITWE LULU......

STAA wa shindano la Tusker Project Fame, Peter Msechu, amechukizwa na hatua ya baadhi ya wapambe wanaompigia simu na kumtaka ampe binti yake jina la Lulu. Msechu alipata mtoto huyo usiku wa Pasaka.

Amesema: Usiku wa Pasaka mimi na mchumba wangu au mke wangu mtarajiwa, tulibarikiwa kupata mtoto wa kike aitwaye Lauren, namshukuru Mungu kwa hilo na nina furaha sana.

"Ila kitu kimoja kilichonikera ni kwamba usiku ule wa Pasaka, Barnaba pia alipata mtoto na akampa jina la Steven, sasa kilichonikera ni kwamba watu kadhaa walinipigia simu na kuanza kuniambia kwamba nimuite mwanangu Lulu.

Lulu ni mwigizaji wa kike mwenye umri wa miaka 17 (kama inavyodaiwa) anayekabiliwa na kesi akituhumiwa kuhusika na kifo cha mwigizaji, Steven Kanumba.
Kifo cha Kanumba kilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Pasaka

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms