Friday, April 6, 2012

.......WANAMITINDO WAPANIA KUFUNDANA.....


WABUNIFU wanne wa mavazi walioshiriki wiki ya mitindo Afrika Kusini wameeleza kufurahishwa kwao na ushiriki wao huo huku wakifafanua yale waliyojifunza wakiwa nchini humo kuwapa na Watanzania wenzao.

Ziara hiyo ya wabunifu kwenda Afrika Kusini, ilidhaminiwa na mwanamitindo mahiri Millen Magese inayelenga kukuza na kutangaza tasnia ya ubunifu wa mavazi na uanamitindo wa Tanzania katika anga la kimataifa kupitia mradi wa Tanzania International Fashion Expose (TIFEX).

Wakizungumza katika nyakati tofauti, wabunifu hao walifafanua kuwa onesho hilo limewafundisha mengi kwa kuwa wamekutana na wabunifu kutoka nchi mbalimbali za ndani na nje ya bara la Afrika.

Mbunifu, Evelyn Rugemalira alisema kuwa amejifunza namna ambavyo wabunifu wa nje wanavyojitangaza na kutafuta soko.

Naye Doreen Noni kupitia lebo yake ya Eskado Bird alisema kuwa mara nyingi amekuwa akishiriki katika maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, mwaka huu ametengeneza nguo za kuvutia zaidi.

Alisema kuwa kupitia onyesho la wiki ya mitindo Afrika Kusini ameshajipatia soko la kimataifa kwa kuwa onesho hilo limemtangaza zaidi.

Akizungumzia hayo, Jamila Vera Swai akishirikiana na Julie Lawrence alisema kuwa kupitia tamasha hili nguo zake zitatambulika kimataifa zaidi na kuweza kumweka katika ramani ya Afrika. Julie kupitia mradi wake wa fahari uliopo kisiwani Zanzibar aliwavalisha vidani na mikoba wanamitindo waliovaa nguo za Jamila.

Kwa upande wa mratibu wa ziara hiyo Millen Magese alisema kuwa. Nimefurahi sana kufanikisha ziara hii kwani mwanzo wa kutangaza kazi zetu kimataifa umeanza vizuri kupitia fani hii ya wabunifu wa mavazi na wanamitindo."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms