Saturday, April 14, 2012

.......NIMEPAGAWISHWA MNO NA GWYNETH PALTROW .........

AMESHAKUWA na wapenzi wengi na wanaume maarufu duniani, lakini inaonekana kwamba Rihanna anaweza kuwaonea wivu hata wanawake wenzake.
Mwanamuziki huyo, ambaye kwa sasa anaipromoti filamu yake ya kwanza kucheza ya Battleship, amekiri kwamba haelewi ni kwa nini anamuonea wivu Gwyneth Paltrow.
Rihanna alishirikiana na mume wa mcheza filamu huyo, Chris Martin na bendi yake ya Coldplay katika kibao chake cha Princess of China.
''Inafurahisha kuona kwamba wanamuziki wengine wanaupenda muziki wako. Kuwa na bendi kama Coldplay - ni jambo zuri sana.
"Tulishirikiana na Coldplay vizuri. Lakini nimepagawishwa mno naye (Gwyneth). Mwili wake. Ninamuonea wivu mno. Sielewi kwa nini nampenda namna hii," alisema kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio cha Australia
.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms