Monday, April 16, 2012

.........NDOA YANGU IKO SHWARI NA IMARA, HAYO MENGINE NI UVUMI TU......

JADA Pinkett Smith amesema uvumi kwamba ndoa yake iko katika hatihati siyo wa kweli na kwamba tetesi hizo zitakwisha punde.

Hivi karibuni ilivumishwa kwamba ndoa yake na William Smith - imevunjika, jambo ambalo mwanamama huyo amelikanusha.

Inaelezwa kwamba uvumi huo umeendelea kutawala kwa takriban mwaka mmoja sasa. Wawili hao walioana mwaka 1997 na wamebahatika kupata watoto wawili - Jaden (13) na dada yake Willow (11).

Nyota hao wameendelea kukanusha uvumi huo kwamba ndoa yao imefika ukingoni baada ya kudumu kwa miaka 14 na sasa Jada Pinkett Smith ameonekana kuchoshwa na ripoti hizo.

"Kila mwaka, wanandoa wawili nyota lazima wawepo kwenye vyombo vya habari kuhusu matatizo ya ndoa yao. Mwaka huu, kwa bahati mbaya, ni sisi! Ninataka kuwaeleza kwamba tulipaswa kuitegemea hali hii," alilieleza jarida la Gala France.

"Lakini Will na mimi tunaujua ukweli. Tunasubiri kwa amani kabisa tufani hii ifikie tamati."

Amesema anaamini tetesi hizo zimeibuka kwa sababu wanatumia muda mwingi wakiwa mbalimbali kutokana na mikataba yao. Lakini Jada amesisitiza kwamba uhusiano wao uko katika hali njema kabisa kwa mumewe na watoto, pamoja na kuwa mbalimbali.

"Tetesi hizo siyo za kweli. Ninasafiri sana kwa sababu ya kazi zangu, kama Will anavyofanya. Ukweli kwamba ninaongozana na binti yetu, Willow, wakati Will anaongoza na kijana wetu, Jaden, hauleti unafuu wa mambo," alisema.

"Lakini maisha yetu hayajabadilika. Hata kabla ya kupata watoto, tulikuwa mbalimbali kila wakati kwa majukumu ya kazi."
Wanandoa hao wanatenga muda wa kuwa pamoja kila wanapopata mapumziko ya kazi zao na hivi sasa anategemea kwenda kwa mapumziko ufukweni.

"Kwa ujumla, Will na mimi huchukua likizo ya miezi miwili, kila mwishoni mwa mwaka," alisema. "Kuanzia ile sikukuu ya Shukrani, hushusha mapazia na hakuna kitu kinachotusumbua hadi Januari."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms