Monday, April 16, 2012

........NAPETA KWA SABABU LUGHA SIYO TATIZO KWANGU.....

MCHEZA filamu wa India, Bipasha Basu, ambaye anatarajia kuanza kuonekana kwa mara ya kwanza Hollywood katika filamu ya Singularity, amesema kwamba lugha siyo kikwazo kwake.

Bipasha, ambaye aliwahi kutajwa kuwa mpenzi wa mwanasoka Cristiano Ronaldo, amesema hakupata shida sana katika uigizaji kwa kikwazo cha lugha, kwani mwigizaji yeyote hawezi kutatizwa na lugha.

Sidhani kama lugha inaweza kuwa kikwazo kwa mwigizaji yeyote hasa kama anataka kufanya kazi yake sawa sawa, alisema na kuongeza kwamba ameweza kucheza ndani ya Bollywood filamu za Bengali pamoja na zile za Kusini, ambazo lugha zinatofautiana.

Kwa kadiri nafasi ninayopaswa kushiriki inavyonivutia, huwa sishindwi kucheza," alisema.

Kuhusu filamu ya Singularity, amebainisha kwamba kufanya kazi kwenye filamu hiyo ulikuwa ni wakati mzuri sana kwake na anasubiri kwa hamu kuanza kuonyeshwa kwa filamu hiyo.

Ni kweli kulikuwa na uchelewaji, lakini filamu itatoka kama ilivyopangwa,alisema na kukanusha madai kwamba filamu hiyo ilikuwa kwenye matatizo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms