Thursday, April 5, 2012

.....NACHUKIA TALAKA - SUSAN PETERS.........

SUSAN Peters mmoja kati ya mastaa wakubwa wa Nollywood, anasema si kweli kuwa wanawake wanakataa kuolewa kwa kuwa hawapendi, isipokuwa wanaogopa talaka.

Anasema, mama yake huwa anamhusia kila siku kuwa makini na mwanamume atakayemuoa, kwa kuwa chaguo baya litampelekea kwenye talaka.

"Nimetoka kwenye familia bora, sijawahi kusikia mtu ameachika au ameacha, yaani talaka kwetu ni jambo ambalo litahitaji maelezo marefu kwa kuwa hakuna kitu kama hicho," anasema Susan.

Aidha anasema hajaolewa mpaka sasa kwa kuwa hajakutana na mwanamume mwenye vigezo vya kuishi naye milele.

"Sijaolewa mpaka sasa kwa kuwa ndoa haijapiga hodi mlangoni kwangu, siku ikifika nitaolewa kwa kuwa natamani sana kuwa ndani ya ndoa," alisema Susan.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms