Tuesday, April 24, 2012

.......MTOTO WA MADONNA ABAMBWA AKIVUTA SIGARA....


NYOTA wa muziki wa pop, Madonna Louise Ciccone amesema ameshtushwa na picha za mwanaye, Lourdes Leon zilizozagaa ambazo alipigwa wakati akivuta sigara akiwa katika matembezi.

Madonna ameapa kufanya kila awezalo kumuachisha binti yake huyo mwenye umri wa miaka 15, huku akisema kitendo hicho kimemuumiza.

Mtoto huyo alipigwa picha akivuta sigara huku akiwa amezungukwa na wavulana katika mitaa ya Jiji la New York mwezi uliopita.

Mwanamuziki huyo amesema kama mzazi, kitendo hicho kumemuumiza na pia binti huyo amefanya kosa ambalo linaweza kumuingiza matatizoni kwa kuwa kwa sheria za Marekani mtu anayeuruhusiwa kuvuta ni yule aliyetimiza umri wa miaka 18.

"Hili litanifanya niwe mkali sasa, kila kitu huwa ninazungumza naye kwa utaratibu, lakini hili la kuvuta sigara sitaweza kulivumilia," anasema Madonna.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms