Sunday, April 29, 2012

...........MR. MISIFA AMWAGA MBOGA........

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes Mr Misifa, ameamua kuingilia kati tabia ya vijana wengi kujikita katika mapenzi ya kwenye mtandao ambayo kwa mujibu wa msanii huyo ni ya kudanganyana.

Dully ambaye hivi sasa ameibuka na wimbo wake mpya 'Mapenzi ya BBM', amesema alisukumwa kuandika mashairi ya wimbo huo kutokana na tabia ya akinadada wengi siku hizo kuutumia mtandao huo kuharakisha ngono kabla ya ndoa.

"Mapenzi ya BBM ni wimbo maalum kwa watu wanaotumia BBM (Blackberry Messenger) tu," alisema.

"Siyo Watanzania wote, lakini wapo wachache wanaoufahamu mtandao huu. Nimeamua kuutoa wimbo huu kutokana na huduma hii ya Blackberry Messenger kushika chati hapa Bongo.

"Yaani mtandao huu umewashawishi akinadada wengi kujiingiza katika masuala ya ngono za mapema ili waweze kupata fedha za kununua simu aina ya Blackberry ili waweze kujiunga katika mtandao huo."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms