Sunday, April 8, 2012

.........MKATABA WAWAWEKA PAMOJA BECKHAM, KATY PERRY NA MESSI.......


MWIGIZAJI, Katy Perry, amejikuta akiwa karibu na David Beckham baada ya kupewa mkataba wa kutengeneza tangazo jipya la Adidas.

Watu hao wameungana na nyota wa Barcelona, Lionel Messi na mchezaji wa basketball, Derrick Rose, katika tangazo hilo ambalo ni mahususi kwa ajili ya matayarisho ya michezo ya Olimpiki ya Juni mwaka huu.

Katika tangazo hilo, Beckham, anaonekana akiwa amevaa nguo za Adidas huku akikimbia pembeni ya mto Thames jijini London na Derrick anaonekana akikimbia katika mitaa ya mji huo pia.

Messi anaonekana akiwa katika mitaa ya nyumbani kwao Buenos Aires akifanya mazoezi makali na
Katy anaonekana akiwa jijini Los Angeles akikimbia ufukweni.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms