Thursday, April 19, 2012

.........MITAANI KUNA WASANII WENGI SANA WENYE VIPAJI.....


MWIGIZAJI wa filamu Swahiliwood Hamida Atosi amesema kuwa mitaani kuna wasanii wengi wenye vipaji lakini bahati mbaya hawapati nafasi ya kuonyesha vipaji vyao hadi pale wanapopata fursa hiyo na kupewa nafasi kubwa kwa ajili ya kuigiza katika filamu husika hali hiyo pia naye ilimpata lakini baada ya kushiriki katika filamu ya Lap Top nyota yake inangara.

Wasanii chipukizi wana uwezo mkubwa lakini ni nani anayeweza kuwaamini kuwa wao ni bora, binafsi nashukru kupata nafasi niliyoigiza katika filamu ya Lap Top lakini pia naona ukuaji wa tasnia ya filamu nchini kutokana na mtayarishaji ambaye ni Gallus Mpepo kuniamini kunipa nafasi kuigiza kama mama maana akina mama Dar ni wengi lakini kaniona mimi ninayeishi Morogoro.

Hamida ni mwigizaji mahiri katika uigizaji nap engine anaweza kuleta upinzani katika nafasi za waigizaji kama akina mama Kawele, Hidaya Njaidi na wengineo wanaotamba katika tasnia ya filamu Swahiliwood, msanii huyo anavuma sana Mkoani Morogoro na ndio filamu hiyo ya Lap Top ilikorekodiwa mwanzo mwisho.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms