Wednesday, April 18, 2012

.....LULU ASHEHEREKEA BIRTHDAY YAKE GEREZANI.......

MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael Lulu jana Jumatatu alitimiza miaka 17 akiwa katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Lulu, ambaye anashikiliwa katika gereza hilo akishtakiwa kwa madai ya kumuua msanii wa filamu Steven Kanumba, Jumatano iliyopita alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu, lakini hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa cheti cha kuzaliwa ambacho Mwanaspoti imekiona, inaonyesha kuwa Lulu alizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Aprili 16, mwaka 1995.

Hiyo ina maana kuwa juzi Jumatatu, Lulu alisherehea siku yake ya kuzaliwa, ingawa hakuna uhakika kama alikula keki gerezani.

Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu amesajiliwa kwa majina ya Diana Elizabeth, huku jina la baba likiwa ni Michael Edward Kimemeta na mama akiitwa Lucresia Agustino Kalugila.

Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu alizaliwa Aprili 16, 1995, lakini alisajiliwa siku tatu baadaye, yaani Aprili 19, mwaka huo.
Lulu, ambaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano iliyopita na kutotakiwa kujibu chochote, alitoa maelezo yake Polisi Jumatatu ya wiki iliyopita ikiwa ni saa 65 tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba Aprili 7.

Lulu alizungumza na kachero wa Makao Makuu ya Polisi ambaye pia ana taaluma ya saikolojia.

Taarifa za uhakika ambazo mwandishi wetu amezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kachero huyo (jina tunalo) alitoka Makao Makuu kusaidia kufanya mahojiano na binti huyo ambaye mtoa taarifa wetu anasema hakuwa tayari kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo, lakini alitumia takribani muda wa saa tatu kumlainisha Lulu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms