Tuesday, April 17, 2012

.......LOL MAGESE HAWATAMBUI WASANII WA KIBONGO......HAHAHAHA......

MWANAMITINDO, Happiness Magese, aliyewahi kuwa Miss Tanzania, hivi karibuni ametoa mpya pale alipoonyesha wazi kutowafahamu wasanii wote wa Swahiliwood zaidi ya wawili tu, yaani marehemu Steven Charles Kanumba na Vincent Kigosi 'Ray'.

Mwanadada huyo ambaye pia alikuwa katika Kamati ya Mazishi ya Kanumba, aliyasema hayo alipozungumza na Mwanaspoti katika makaburi ya Kinondoni wakati wa mazishi hayo.

Happines alimuona msanii Irene Uwoya kazimia akashangaa na kuuliza ni msanii gani huyo?

Mimi siwajui kabisa wasanii wa Kitanzania zaidi ya huyu marehemu kwa sababu alikuja Afrika ya Kusini na nikakutana naye," alisema.

Nakumbuka nilibadilishana naye mawazo, unajua mimi sipo hapa kwa muda mrefu na sijabahatika kuweza kuangalia sana filamu za hapa nyumbani.

Ninaowafahamu zaidi ni wanamitindo kwa sababu nipo karibu nao, lakini kwa filamu labda wachache sana kama Kanumba na Ray hakuna wengine zaidi yao.

Mwanamitindo huyo ambaye anafanya shughuli zake nchini Afrika ya Kusini pia alishiriki vema katika kamati ya mazishi ya Kanumba kwa kutoa mchango mkubwa na kupanga mambo mbalimbali yaliyowezesha kufanikisha mazishi.

Alisema pamoja na kuwa amekuwa si mpenzi wa filamu hizo, lakini anawapenda wasanii wote na hasa wale ambao anakutana nao na kubadilishana nao mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Kwa sasa mwanadada huyo yupo jijini Dar es Salaam kwa mapumziko.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms