Monday, April 23, 2012

..........KIM KARDASHIAN AGEUKIA SIASA.........


KIM Kardashian amejipanga kujiongezea uwanja mwingine wa kujionyesha kwani amesema ndani ya miaka mitano ijayo anataka kutimiza ndoto yake ya kuingia katika siasa.

Katika kipindi cha Keeping up With Kardashians, Kim amesema anataka kugombea Umeya wa Jiji la Glendale katika uchaguzi ujao.

Kim, mwenye umri wa miaka 31, alimwambia ndugu yake Kloe kuwa anatarajia kununua nyumba katika mji huo ili waanze kuishi huko na kujitengenezea mazingira ya ushindi.

Hata hivyo, Kim amekosolewa kwa kutaka kujiingiza kwenye siasa wakati hazijui hata kidogo. Inaelezwa kuwa hakuna nafasi ya Umeya katika Jiji la Glendale. Jiji hilo linaongozwa na wajumbe watano wa Halmashauri.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms