Mahakama
ya hakimu mkazi KISUTU jijini Dar es Salaam leo imeahirisha kesi ya
tuhuma za mauaji inayomkabili ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ dhidi ya
aliyekuwa mwana filamu mahiri Marehemu STEVEN KANUMBA.
Wakili
wa Upande wa Serikali ELIZABETH KAGANDA akizungumza mahakamani hapo
amedai Upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba kesi hiyo itatajwa
tena mei 7 mwaka huu.
Umati
mkubwa ulijitokeza katika mahakama hiyo kwa lengo la kufuatilia mwenendo mzima
wa kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi hapa nchini.
Hii
ni mara ya Pili kwa ELIZABETH MICHAEL kupandishwa Kizimbani kosa la
mauaji ya mwana filamu huyo mnamo April 7 mwaka huu eneo la Sinza
Vatican Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment