Saturday, April 14, 2012

........HUO NI UZUSHI SISI HATUJAFA TUKO MITAANI TUNADUNDA.........

WANAMUZIKI nyota wa Marekani, Justin Bielber, Usher Raymond na Eminem wamekanusha uvumi ulioenezwa kwa nyakati tofauti kwamba wamekufa katika matukio kadhaa ya ajali.

Uvumi huo wa vifo vya mastaa hao unaonekana kufagiliwa na mashabiki wengi, hasa watumiaji wa mtandao wa Twitter, ambapo umekuwa ukitolewa kila wakati na kuwafanya mashabiki wengi duniani kutuma salamu za rambirambi.

Nyota wa R'n'B Usher Raymond wiki hii ndiye alikuwa mhanga wa mwisho kuzushiwa kifo kufuatia ripoti zilizosambazwa mtandaoni kwamba amekufa kwenye ajali ya gari.

Mwanamuziki huyo alilazimika kujibu haraka haraka na kutuma picha zake mtandaoni, ili kuthibitisha kwamba alikuwa mzima wa afya na wala hakuwahi kupata ajali.

Usher siye pekee aliyepatwa na dhahama hiyo katika ulimwengu wa uvumi wa vifo vya mtandaoni. Britney Spears, Adele na Eminem pia wamewahi kuzushiwa vifo - ambavyo cha kuchekesha ni kwamba vyote vilidaiwa kutokana na ajali za barabarani.

Chris Brown aliwahi kuchanganyikiwa baada ya mtu mmoja kutuma ujumbe kupitia Twitter na Youtube akitoa rambirambi na maneno kama "RIP Chris, utakuwa ukiwadunda wanawake huko ahera kuanzia sasa hata milele."

Kali zaidi ilikuwa ya mwanamuziki na mwigizaji, Jon Bon Jovi, ambaye ripoti zilisema alifia hospitali baada ya kukutwa akiwa mahututi kutokana na ugonjwa wa moyo.

Jovi aliuona uvumi huo mtandaoni na kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook huku akibandika na picha aliyoshikilia bango lililosomeka: "Mbinguni kunafanana kabisa na New Jersey!" halafu akaandika kwamba ilikuwa ni Desemba 19, 2011 saa 12:00.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms