Wednesday, April 25, 2012

......HEE MAINDA ANA UJAUZITO????.......HAHAHAHA.....

MWIGIZAJI nyota wa Swahiliwood, Ruth Suka Mainda amedai kukumbwa na usumbufu kutoka kwa wadau na wapenzi wa filamu baada ya kupigiwa simu nyingi huku kila mpiga simu akitaka kujua kuhusu ujauzito wake.

Mainda amesema, tukio hilo limejitokeza hivi karibuni kwa baadhi ya watu kumpigia simu wakitaka kujua kama kweli ni mjamzito.

Ninasumbuliwa sana na watu wakitaka kujua kama kweli mimi ni mjamzito, na ukichelewa kumjibu mtu ukiwa umeduwaa, swali linalofuata kabla hata ya kujibu anakuuliza je, baba wa mtoto ni nani? Jibu ni kwamba, mimi si mjamzito bali ni filamu tu, anasema Mainda.

Mainda anafafanua kuwa, wengi wanampigia simu kutokana na picha alizopiga akiwa anarekodi filamu yake mpya ya Mke Mwema ambayo kaigiza kama mama mjamzito mwenye matatizo na picha hizo kuchukuliwa na watu ambao wanatangaza kuwa yeye ni mjamzito.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms