Sunday, April 8, 2012

......BALOTELI ANAKIRI KUTEMBEA NA CHANGUDOA WA ROONEY.....

NYOTA mtukutu wa Manchester City, Mario Balotelli, wiki hii ameibuka na kuanika hadharani kwamba aliwahi kufanya mapenzi na mmoja kati ya machangudoa waliowahi kulala na Wayne Rooney.

Balotelli alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Jenny Thompson.
Mchezaji huyo raia wa Italia mwenye umri wa miaka 21, alikiri kwamba alilala na mwanamke huyo katika nyumba yake yenye thamani ya pauni 3 milioni huko Cheshire na hakutaka kumpeleka changudoa huyo hotelini.

Naye Jenny alikiri kwamba alilala na mwanaume huyo huku mpenzi wa Balotelli aitwaye Raffaella Fico akiwa Italia.

Jenny alisema kuwa alikutana na Balotelli katika sherehe ya kuzaliwa ya kaka wa mchezaji huyo aitwaye Enoch na wakaishia nyumbani kwake.

Alisema: Tulipokuwa katika nyumba yake, aliniuliza kama ninataka kwenda chumbani kwake. Baada ya muda tulijikuta kitandani."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms