Friday, April 20, 2012

............AFYA YA SAJUKI NI TATA........UKWELI ni kwamba, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ anaumwa, Ijumaa limemshuhudia na linakuhabarisha.
Hali ya Sajuki imeendelea kuwa mbaya akidhoofu mwili siku hadi siku kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa.
Aprili 15, mwaka huu Sajuki na mkewe Wastara Juma walifanya sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen ambayo ilihudhuriwa na waandishi wetu waliomshuhudia msanii huyo akiwa amedhoofu sana.
WASANII WAMTOLEA MACHOZI
Kabla ya kuugua, Sajuki alikuwa mwanaume aliyeshiba (mnene) na mwenye nguvu hivyo kutokana na hali yake ilivyobadilika na mwili kuwa mdogo, baadhi ya wasanii waliofika kwenye sherehe hiyo walijikuta wakimtolea machozi.
“Jamani tuacheni utani, Sajuki anaumwa sana na anahitaji msaada na maombi yetu ili arejee kwenye hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa waigizaji wenzake.
SAJUKI KURUDI INDIA
Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
WADAU TUMSAIDIENI SAJUKI
Kufuatia hali ilivyo, BLOG hili inaomba wadau tujitokeze kumchangia Sajuki fedha kwa ajili ya matibabu kupitia simu ya mkononi kwa kutuma kwenye Tigo Pesa namba 0713 666 113 au kwenye akaunti namba 050000003047 katika Benki ya Akiba Commercial yenye jina la Wastara Juma Issa.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms