Sunday, April 29, 2012

,,,,,,,,, AFANDE SELE ATOA SOMO KWA WASANII KUHUSU KIFO........

MFALME wa Rhymes kutoka mji kasoro bahari, Morogoro, Afande Sele, amewatahadharisha wasanii wenzake kuwa makini na maisha akiwaambia kuna siku ya kufa kama ilivyo ile ya kuzaliwa.

Afande Sele ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa Aprili 24 mwaka huu, amewataka wasanii na Watanzania kwa ujumla kuishi maisha ya amani na upendo.

"Tuna wajibu wa kukumbuka kuwa kama kuna kuzaliwa basi kuna kufa vilevile. Siku ya kuzaliwa itumike kama changamoto kwetu tukitafakari kwanini tupo duniani na makusudi na Mungu kutuumba wanadamu na si wanyama au ndege," alisema.

Afande Sele anakumbukwa sana kwa albamu nne alizowahi kutoa tangu alipojiingiza katika sanaa ya muziki miaka ya tisini.

Albamu hizo ambazo ziliweza kuwashika watu kwa vipindi tofauti ni Mkuki Moyoni, Darubini Kali, Nafsi ya Mtu na Heshima.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms