Thursday, March 1, 2012

......WIVU WA MAPENZI UNANUTESA..........

KINARA wa bongo movie, Salma Jabu ‘Nisha’, amedai kuwa huwa anajisikia vibaya pale anapopiga simu ya mpenzi wake na kuambiwa iko bize muda wote kitu ambacho kinafanya kusia anazungumza wanawake wengine.

Msanii huyo alitoa kauli hiyo inayotafsiliwa kuwa ni wivu wa mapenzi, baada ya mwandishi wa habari hizi, kuzungumza naye juu ya tatizo kubwa linalilosababisha kumuonea wivu mpenzi wake.

Alisema kuwa anajisikia kuumia kwa sababu anahitaji kuzungumza na mpenzi wake muda fulani lakini wakati huo ukifika anapopiga simu anaambia inatumika na anahisi tayari aanaibiwa na wanawake wengine.

“Naweza kusema kwamba naumia kwa sababu unapiga simu ya mpenzi wako tena unakuta iko bize kwa kweli huwa nawaza mambo mengine ambayo siyo kweli,” alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms