Tuesday, March 20, 2012

..........WANAFUNZI WA UDOM WAMENIFURAHISHA KWA ZIARA YAO HII YA KUTOA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI ........


Mmoja wa Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akishusha Baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wakati wanafunzi wa UDOM walipowasili Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo Manispaa ya Dodoma Mjini mchana wa leo 

Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Areman Kaziguto (mwenye fulana nyeupe) akitoa maelezo machache mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya viwandani iliyopo manispaa ya Dodoma mjini ambapo wanafunzi wa UDOM leo walifanya ziara na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia Usafi 


Mwalimu wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani Bi Ester Bahati akitoa shukrani za dhati kwa wanafunzi wa UDOM waliotembelea Shule hiyo na Kutoa Misaada ya Vifaa vya Kufanyia Usafi leo Mchana 
Picha hapo juu ni Mwanafunzi wa UDOM Josephat Lukaza akitoa Maelezo jinsi ya matumizi sahihi ya vifaa vya kufanyia na kutunzia uchafu kwa wanafunzi wa klabu ya mazingira ya shule ya sekondari ya viwandani iliyopo Dodoma mjini

Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo kwenye manispaa ya Dodoma wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) waliotembelea Shule hiyo Mchana wa leo.Picha Zote na Josephat Lukaza

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms