Friday, March 30, 2012

....USIPO JIFAGILIA WEWE ATAKUFAGILIA NANI???..........

MWIGIZAJI wa filamu Swahiliwood, Patrick Herman Zungu, amesema kuwa katika filamu za mapigano anaamini kuwa hana mpinzani na anasema filamu alizoigiza zimefanya vizuri na kupendwa watazamaji.

Msanii huyo ameshiriki zaidi ya filamu 16 ambazo tayari zimetoka.

Kwanza kabisa sura yangu pekee yake ni mauzo, ilitakiwa niende kuigiza katika filamu kubwa za kimataifa kutokana na muonekano wangu jinsi nilivyo.

"Jambo lingine, mimi ni mtu wa mazoezi kwa hiyo ninavyoigiza filamu ya mapigano napigana kweli na si utani, anasema Zungu.

Msanii huyo mwenye muonekano wa kishababi yuko katika maandalizi ya filamu ya mapigano ambayo ameshindwa kutaja jina kwa usalama wa filamu yao.

Zungu ameigiza filamu kama Ushanga wa Ajabu, Back from Hell, Action number One, Filamu ya Mama, Dinyilu, Reason, Latifa, Mateso ya Jini, ambapo katika filamu zote hizo amecheza kama adui na mtu katili asiye na huruma.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms