Thursday, March 29, 2012

.....STEVE NYERERE AMCHANA JB......

MWIGIZAJI wa filamu Swahiliwood, Steven Mangere Steve Nyerere, katika hali ya masihara alitumia muda huo kumpiga dongo msanii mwenzake ambaye ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Club, Jacob Stephen JB kwa kueleza kuwa JB pamoja na kumiliki kampuni na sasa ni kinara wa mauzo, lakini kampuni yake haina hata ofisi kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, tofauti na nyota wenzake kama Ray, Kanumba na Mtitu na Richie.

Steve Nyerere, msanii mwenye staili yake ya kipekee katika kujitafutia fedha ambaye awapo kazini yupo tayari kufanya jambo lolote ili apate pesa, alimshushia madongo hayo wakati wa sherehe za Bongo Movie Club kutimiza mwaka mmoja wa kuundwa kwake. Kundi hilo linaundwa na wasanii nyota na chipukizi.

JB bonge la mume, bonge la bwana, tumbo kubwa lakini pamoja na kumiliki tumbo ndiye msanii asiyekuwa na ofisi, huyu anampenda na kumheshimu mkewe, lakini jamaa hana ofisi kwa ajili kampuni yake, Steve alisema hayo huku akicheka.

Msanii huyo alizidi kusisitiza kuwa alikuwa akitania katika kuwataja wasanii na kuoanisha na matukio yao ya kweli huku akisema; "Leo nawatuza wasanii kulingana na matukio yao, leo nawapa tuzo zao kwa matukio yao, si unaona kama JB hana ofisi, msanii mkubwa huyo,alimalizia.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms