Thursday, March 8, 2012

...........SOMALIA YAOMBA KUJIUNGA NA JUMUIA YA AFRICA MASHARIKI.....


Moja kati ya stori kubwa za leo ni kuhusu nchi ya Somalia ambayo imekua ikijaribu kujikwamua kutoka kwenye vita vya miaka 20, kutuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, imethibitisha kupokea maombi ya Somalia huku Taarifa kutoka serikali ya mpito ya Somalia zikiamplfy kwamba wameamua kujiunga na jumuiya hiyo kutokana na usalama kuimarika na utulivu kuanza kupatikana.
BBC wameamplfy kwamba Somalia inakuwa nchi ya tatu baada ya Sudan Kusini na Sudan kaskazini kutuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki ambapo Hata hivyo mpango wa Sudan kutaka kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki umekataliwa.
Kwa sasa jumuiya ya Afrika Mashariki inajumuisha nchi tano, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi ambapo Mbali na nchi wanachama kuwa na ruhusa ya kufanya biashara bila vikwazo vyovote, kwa wakati huu zinapanga kuwa na sarafu moja kufikia Juni mwaka huu

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms